Wabunge waghadhabishwa na ununuzi wa mfumo mpya wa SHIF

  • | Citizen TV
    114 views

    Wizara ya afya ina mpango wa kununua mfumo wa otomatiki wa bima mpya ya afya ya jamii ,SHIF, kwa shilingi bilioni 4. Hayo ni kwa mujibu wa katibu katika wizara ya afya Harry Kimtai aliyeiambia kamati ya bunge kuhusu afya kuwa mchakato wa ununuzi unaendelea. hatua hiyo imeighadhabisha kamati hiyo ikisema kuwa pia bima ya afya ya NHIF ilikuwa na mfumo kama huo na kwamba utaratibu ufaao haukufuatwa.