Wabunge wanawake walalamikia mpango ulisitishwa kuhusiana na mpango wa Linda Mama

  • | Citizen TV
    76 views

    Wabunge wanawake sasa wanataka waziri wa afya Susan Nakhumicha atimuliwe kazini hasa kwa kusitisha mpango wa Linda Mama uliokuwa unawasaidia kinamama wanaojifungua kutoka familia za mapato ya chini. Wakizungumza nje ya majengo ya bunge, wabunge hao walilalamika kuwa wanawake wengi wameteseka kutokana na kuondolewa kwa mpango huo na upo uwezekano wa vifo vya mama na mtoto kuongezeka iwapo hautarejeshwa haraka.