Wabunge wataka chama cha ODM kumchukulia hatua ya kinidhamu mbunge wa Homa Bay Peter Kaluma

  • | K24 Video
    40 views

    Wabunge chini ya muungano wa mtandao wa wabunge wa Afrika wamekitaka chama cha ODM kumchukulia hatua ya kinidhamu mbunge wa Homa Bay Peter Kaluma kufuatia mswada wake wa marekebisho unaokusudia kuruhusu maafisa wa serikali kushikilia ofisi za umma baada ya kuhudumia kifungo kwa tuhuma za ufisadi. Kaluma anataka mabadiliko ya sheria ya kuhalalisha ufisadi na uhalifu wa kiuchumi ya mwaka 2003 kwa kuondoa kabisa kifungu cha 64 kwenye sura ya sita ya katiba ambayo inawazuia wahusika wa ufisadi na uhalifu wa kiuchumi kushiriki uongozi wa afisi za umma. Kulingana na kundi hilo marekebisho ya kaluma ni kinyume na maadili ya ODM ambayo kinara wake amekuwa mstari wa mbele barani kupinga ufisadi.