- 260 viewsDuration: 5:02Viongozi kaunti ya Taita Taveta wametakiwa kushirikiana na wamiliki wa shamba la kijamii la Kishushe ili wachimbaji madini wadogo wanufaike na raslimali hiyo. Kulingana na viongozi wa shamba hilo , madini hasa ya chuma, ni sharti yaanze kuchimbwa kupitia ushirikiano na wawekezaji mbalimbali wa kibinafsi. wakazi wanaitaka wizara ya madini kuharakisha kutoa leseni za uchimbaji madini kwa wafanyabiashara wadogo.