Wafanyabiashara katika mji wa Hola, kaunti ya Tana River wamepinga mswada wa fedha wa mwaka huu wa kaunti hiyo, wakisema mapendekezo yake yataharibu biashara ndogo ndogo ambazo tayari zinakabiliana na changamoto kubwa za kiuchumi. Kwa upande mwingine, mamia ya wanawake wajawazito kutoka Embu na kaunti jirani wamenufaika na kambi ya matibabu ya bila malipo iliyoratibiwa na hospitali ya Neema Universal Healthcare kusaidia kupunguza vifo vya kina mama wakati wa kujifungua.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive