Skip to main content
Skip to main content

Wafanyabiashara wa Ringa walalamikia uvamizi wa nyuki

  • | Citizen TV
    1,675 views
    Duration: 2:14
    Wafanyabiashara katika Soko la Ringa, Kaunti ya Homa Bay, sasa wanaitaka idara ya kilimo ya kaunti hiyo kutatua tatizo la nyuki ambao wamekuwa wakiwahangaisha kwa miezi kadhaa. Nyuki hao wamejenga makazi kwenye vigingi vya umeme sokoni humo na huwavamia wateja mara kwa mara. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, wafanyabiashara hao wanadai kuwa watu wawili wamefariki baada ya kushambuliwa na nyuki, huku wengine wakiuguza majeraha.