WAFANYABIASHARA WAHIMIZWA KUCHUKUA MIKOPO

  • | KNA Video
    22 views
    Wafanyabiashara katika kaunti ya Kilifi wamehimizwa kukumbatia uchukuaji wa mikopo ili waweze kupanua biashara zao. Akizungumza mjini Kilifi katika hafla ya ufunguzi wa tawi la 96 la Benki ya Family mkurugenzi wa shirika la Kenya National Chamber of Commerce Vincent Mwakio amesema kuwa iwapo mfanyabiashara yeyote ana maono ya mbeleni kuhusu biashara yake ni lazima achukue mkopo ili kuendeleza biashara hiyo.