Wafanyikazi 4 wa hazina kitaifa wamekamatwa

  • | Citizen TV
    1,958 views

    Tume ya maadili na kupambana na ufisadi (EACC) imewatia mbaroni wafanyakazi wanne wa hazina ya kitaifa kufuatia madai ya kupokea hongo. Hayo yakijiri huku viwango vya rushwa nchini vinaendelea kupanda kwa kasi, ripoti ya shirika la transparency international ikionyesha kuwa mkenya mmoja kati ya wawili wanaotafuta huduma za serikali hulazimika kulipa hongo. Idara ya polisi inaongoza kwa kudai rushwa kutoka kwa wakenya, ikifuatwa na idara ya ardhi na ile ya utoaji wa leseni za magari.