Wafanyikazi wa kampuni ya sukari ya Nzoia wajitolea kupanda miwa katika shamba la kampuni hiyo

  • | K24 Video
    38 views

    Kutokana na upungufu wa malighafi kwa kampuni za sukari kote nchini, bei ya sukari imeongezeka maradufu. Ongezeko hilo limefanya serikali itangaze mpango wa kuagiza sukari nchini ili kupunguza mzigo wa gharama. Hayo yakijiri, katika kaunti ya Bungoma, wafanyikazi wa kampuni ya sukari ya Nzoia wamejitolea mhanga kupanda miwa katika shamba la kampuni hiyo kutokana na uhaba huo