- 316 viewsDuration: 2:33Wafugaji wa mbuzi waliouza mifugo yao katika soko la mbuzi la Kimalel mwezi disemba wamelalamikia kutopewa malipo yao, takriban miezi miwili baada ya mifugo yao kuuzwa. Wanatishia kuandamana hadi katika ofisi za gavana wa kaunti hiyo kushinikiza malipo yao au warejeshewe mbuzi wao. Wafugaji hao wanadai matapeli waliingilia soko hilo na kujilipa kabla ya wafugaji halali kulipwa.