- 211 viewsNaibu Rais Profesa Kithure Kindiki amewaahidi wafugaji kuwa serikali inaweka mikakati ya kudhibiti wizi wa mifugo. Akizungumza kwenye sherehe za kitamaduni za Loiyangalani kaunti ya Marsabit, kindiki amewataka maafisa wa usalama kukaza kamba ili kuangamiza ujambazi huku akiahidi kubuniwa kwa maeneo zaidi ya utawala ili kuimarisha doria ya polisi.