Wachezaji wastaafu wa Harambee Stars wakiongozwa na kocha mzoefu John Bobby Ogola walishiriki mchuano wa Igaming Africa Summit uliofanyika katika uwanja wa Goan Gymkhana mtaani Parklands hapa jijini Nairobi.
Wengine walioshiriki mchezo huo ni aliyekuwa mlinda lango Matthew "Ottamax" Owino, Patrick Oboya, Ezekiel Odera, na Kepha Aswani. Afisa mkuu mtendaji wa Sofapaka Herbert Kungah aliongoza timu yake ya Rhino kuishinda Elephant mabao 2 kwa 1 katika fainali. Rhino walituzwa shilingi laki moja. Dhamira ya mchuano huu ni kuchangisha fedha za kujenga vyoo katika mitaa ya mabanda.