- 438 viewsDuration: 3:46Wagonjwa wa macho katika kaunti ya Busia na nchi jirani ya Uganda wamepata afueni kufuatia uzinduzi wa kliniki maalum ya magonjwa ya macho yanayolenga kuwahudumia wagonjwa hao kwa bei nafuu. Idadi ya wagonjwa wa macho na hata wanaoopteza uwezo wa kuona ikiongezeka mno katika kaunti ya Busia, wakazi wametakiwa kutafuta matibabu kwa muda ufaao, kwani wengi wao hufika hospitalini baada ya kuathirika vibaya.