Wakaazi katika eneo la Lari walalamikia kupuuzwa kwa barabara za Mau Mau

  • | Citizen TV
    87 views

    Katibu mkuu wa wizara ya barabara Joseph Mbugua ameongoza ziara ya kukagua ujenzi wa barabara katika eneo la Lari kaunti ya kiambu. Ziara hiyo inafanyika wakati kukiwa na shinikizo kutoka kwa wakaazi kuwa baadhi ya barabara hazijawahi kutengenezwa au kukarabatiwa tangu enzi za utawala wa mkoloni na vita vya maumau. Kulingana na mbunge wa lari Mburu kahangara ujenzi wa barabara hizo utasaidia kufungua eneo hilo na kusaidia kufanikisha maendeleo na biashara.