Wakaazi wataka polisi wa akiba waajiriwe West Pokot kuimarisha usalama huko

  • | Citizen TV
    108 views

    Ukosefu wa polisi wa akiba katika kaunti ya Pokot Magharibi umechangia pakubwa misururu ya uvamizi katika maeneo ya mpakani huku wakazi wakiitaka wizara ya usalama wa ndani kuajiri askari hao wanaoishi na wakazi ili kushugulikia maswala ya usalama ya dharura. Wakazi wanasema askari hao wameajiriwa na kusaidia pakubwa katika kaunti za Baringo, Elgeyo Marakwet na Turkana huku kaunti ya Pokot Magharibi ikikosa huduma hiyo muhimu.