- 182 viewsDuration: 3:07Wakazi wanaopakana na ziwa Viktoria sasa wametakiwa kuzingatia usafi wa mazingira ili kuhifadhi ubora wa ziwa hilo. Akizingumza wakati wa ufunguzi rasmi wa makao makuu ya LVBC huko Kisumu, waziri Beatrice Askul alitaja umuhimu wa ziwa hilo katika uchumi wa taifa kutokana na uvuvi pamoja na utalii. Na Kama anavyoarifu Laura Otieno haya yanajiri wakati ambapo idadi ya samaki imeripotiwa kupungua maradufu ziwani humo.