Wakazi takriban 300,000 wa kisiwa cha Mayotte katika Bahari ya Hindi chakabiliwa na uhaba wa maji

  • | VOA Swahili
    530 views
    Wakazi karibu laki tatu wa kisiwa cha Ufaransa cha Mayotte katika Bahari ya Hindi kinachodaiwa na Comoros, wanalalamika kutokana na ukosefu wa huduma ya maji baada ya miezi kadhaa ya ukame. Kisiwa hicho kinakabiliwa na hali mbaya ya ukame kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 30 na mamlaka ya maji yanakata huduma kwa siku mbili kati ya kila siku tatu kutokana pia na matatizo ya mitambo ya maji iliyochakaa. Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali. #wakazi #ufaransa #kisiwa #mayotte #bahariyahindi #comoros #maji #ukame #mamlaka #mitambo #voa #voaswahili #dunianileo - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.