Wakazi wa Bamburi wasema ardhi ya umma imenyakuliwa

  • | Citizen TV
    359 views

    Mzozo wa ardhi umeibuka baina ya serikali ya kaunti ya Mombasa, umma na mwekezaji mmoja kuhusu kipande Cha ardhi, kinachodaiwa kunyakuliwa huko bamburi . Baadhi ya wakazi pamoja na viongozi wa eneo hilo wanadai ardhi hiyo ni mali ya umma, na kuwa tayari serikali ya kaunti inapania kujenga choo cha umma katika sehemu hiyo. Wakaazi wamedai kuwa mwekezaji wa kibinafsi amejenga katika eneo la mkondo wa maji na kusababisha mafuriko. hata hivyo, mwekezaji huyo amekana na kudai kuwa kaunti ya Mombasa ndio iliwauzia ardhi hiyo.