Wakazi wa Bula Towfiq, Garissa, waandamana kwa kukosa umeme

  • | Citizen TV
    544 views

    Wakazi wa kijiji cha Bula Towfiq viungani mwa mji wa Garissa wamefanya maandamano kushinikiza kampuni ya Kenya Power kuunganisha kijiji hicho na nguvu za umeme. Wakazi hao wanasema licha ya hao kupeleka maombi yao kwa ofisi za kampuni hakuna chochote kimefanyika huku shule za eneo hilo pia zikiathirika. Wanasema hali hii imechangia kuongezeka kwa visa vya utovu wa usalama kutokana na giza inayoshuhudiwa nyakati za usiku. Imewalazimu baadhi ya wakazi kugeukia mitambo ya kutumia miale ya jua ambayo pia wanasema haitoshelezi mahitaji yao.