Wakazi wa Eneobunge la Kimilili katika Kaunti ya Bungoma wanalalamika kuwa wawekezaji wa kibinafsi wamevamia na kunyakua kipande cha ardhi cha ekari 1.2 kinachomilikiwa na Shirika la ufadhili wa Kilimo (AFC).
Haya ni huku Tume ya Maadili na Kukabili ufisadi (EACC) ikianza uchunguzi kuhusu malalamishi yao. Wakazi hao wanalalamika kuwa wawekezaji wa kibinafsi wamevamia na kunyakua kipande cha ardhi cha ekari 1.2 kinachomilikiwa na AFC. Wanadai kuwa waporaji hao wameanza shughuli za kibiashara katika ardhi hiyo, ikiwemo ujenzi wa kituo cha mafuta, na pia kuzuia njia ya umma kuelekea Kituo cha Polisi cha Kimilili. Kesi kuhusu ardhi hiyo imeratibiwa kusikizwa tarehe 5 mwezi Machi mwaka huu.