Wakazi wa Soi Nandi wanalalamikia ubovu wa barabara

  • | Citizen TV
    468 views

    Wakazi wa soi eneo bunge la Aldai kaunti ya Nandi, wanalalamikia ubovu wa barabara ambayo wanasema haipitiki. Wakazi hao ambao wanaoishi kwenye mpaka wa Nandi na Kisumu wanasema kuwa wanateseka Kila mara kutokana na hali mbovu ya barabara hiyo huku wakitaka wadau kuhakikisha kuwa barabara hiyo inakarabatiwa haraka iwezekanavyo.Wakizungumza eneo la soi,wakazi walisema kuwa shughuli za uchukuzi eneo hilo zimetatizika pakubwa wakikabiliwa na hali ngumu kutafuta huduma muhimu kutokana na ubovu wa barabara hiyo.