Skip to main content
Skip to main content

Wakazi waandamana wakiilaumu seneti kwa kutotatua mzozo wa ardhii Olderkesi Narok

  • | Citizen TV
    104 views
    Duration: 1:38
    Wenyeji eneo la Enkeroi-Olderkesi wadi ya Nairarra eneo bunge la Narok Kusini wameandamana kuelezea masikitiko ya Kamati maalum ya Seneti inayohusika na Ardhi kudaiwa kufeli kuhudhuria rasmi kikao maalum nao ili kutoa Suluhu ya kudumu ya mzozo wa ardhi. Wakizungumza na wanahabari baada ya maandamano hayo, wamedai kuwa Kamati hiyo kupitia barua rasmi ilipaswa kufika eneo lao tarehe 13 Feburuari mwaka huu kama ilivyoratibiwa ila ikaahirisha bila mawasiliano rasmi. Pia wenyeji hao wamewarai Gavana wa Narok Patrick Ole Ntutu na Mbunge wa Narok Magharibi Gabriel Ole Tongoyo kuingilia kati na kuzungumzia swala hilo waziwazi.