Skip to main content
Skip to main content

Wakazi wapewa hamasisho kuhusu usalama Nyali

  • | Citizen TV
    205 views
    Baadhi ya wakazi, wahudumu wa bodaboda wameanzisha hamasisho kuhusu usalama baada ya vitengo vya usalama kuapa kupambana na magenge ya wahuni yanayowavamia wakazi. Wakiongea eneo la nyali wakati wa siku ya kwanza ya hamasisho hilo, wamiliki wa bodaboda wametaka asasi za usalama kusaidiana nao ili kuwakamata wahuni wakisema pia wao wamekuwa wakilengwa hasa nyakati za usiku. Baadhi ya wazazi wameunga mkono agizo lililotolewa na kamanda wa polisi pwani Ali Nuno wakisema wazazi wengi wameshindwa kuwajibika na kusababisha kuchipuka tena kwa magenge.