- 742 viewsDuration: 3:39Wakazi wa Nanyuki wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya ukosefu wa maji, hali iliyosababisha changamoto za kiafya katika baadhi ya maeneo ya mji. Kufuatia mradi wa maji unaotekelezwa na Kampuni ya Usambazaji wa Maji ya Nanyuki, mradi huu ambao umefikia asilimia 98 kukamilika unalenga kuongeza usambazaji wa maji hadi lita milioni sita kwa siku ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka kutokana na ukuaji wa kasi wa mji wa Nanyuki.