Wakenya 409 wasafirishwa kutoka Sudan huku serikali ikiendelea na mipango ya kuwarejesha nyumbani

  • | Citizen TV
    937 views

    Wakenya 409 wamesafirishwa kutoka nchini Sudan kufikia sasa huku serikali ikiendelea na mipango ya kuwarejesha nyumbani Wakenya waliosalia nchini humo. Waziri wa Maswala ya Kigeni Dkt. Alfred Mutua amesema hayo huku akiongezea kuwa Kenya inahusika pakubwa katika juhudi za kurejesha amani nchini humo. Aidha aliongeza kuwa Rais William Ruto aliongoza mkutano uliohudhuriwa na waakilishi wa Umoja wa matifa kuhusu jinsi ya kupeleka usaidizi nchini Sudan.