Wakili Francis Okomo Okello amezindua tawasifu yake "Concert of Life: From the lakeshore to the boardroom' ambapo ameangazia safari yake kutoka kijijini hadi kwenye meza ya uongozi wa mashirika mbalimbali humu nchini na kwingineko.
Okello anatafakari kuhusu hatua muhimu alizopiga katika sekta za sheria na biashara, kando na kuangazia chimbuko lake na familia yake. Kitabu hicho chenye kurasa mia nne pia kinaangazia hali ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi nchini.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa tawasifu yake hapa jijini Nairobi, Okello aliwataka wajasiriamali na wafanyibiashara kujielimisha zaidi ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali za dunia.