- 4,801 viewsDuration: 48sKesi imewasilishwa mahakamani kutaka kupigwa marufuku kwa Ikulu ya Rais kwa matumizi ya shughuli za kisiasa. Wakili wa maswala ya kikatiba na haki Lempaa Suyianka kwenye kesi yake anasema kuwa, pesa za umma zimekuwa zikitumika kuendeleza ajenda za chama cha UDA katika ikulu. Kesi hii ikimshtaki Mwanasheria mkuu, Msimamizi wa ikulu, chama cha UDA na Rais William Ruto. Mbali na kutaka utumizi wa ikulu kwa shughuli za siasa kuwa kinyume na katiba, pia ametaka vyama vyote vya kisiasa kupigwa marufuku dhidi ya kufanya mikutano yake Ikulu