- 192 viewsDuration: 1:42Wakulima katika Kaunti ya Tharaka Nithi wanahimizwa kuongeza uzalishaji wa alizeti ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka kutoka Chuka Technical and Vocational College, ambayo inaongeza thamani ya zao hilo kwa kuligeuza kuwa mafuta ya kupikia na chakula cha mifugo. Kwa sasa, taasisi hiyo inahitaji takribani tani tano za alizeti, lakini hupata tani moja pekee kutoka kwa wakulima wa eneo hilo, hali inayolazimisha kutafuta mazao hayo kutoka nje ya kaunti.