Wakulima kutoka Kajiado Kaskazini wamehimizwa kupanda mazao yanayostahimili ukame, nyasi za mifugo, na kufanya kilimo mseto ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga.
Katika mkutano wa kupanga mikakati ya msimu wa mvua, ambao ulihudhuriwa na watabiri wa hali ya anga, na washikadau mbalimbali, Wakulima walihimizwa pia kuwekeza katika mbinu za kuhifadhi maji ili kuyatumia katika miradi ya kilimo na kwa matumizi ya nyumbani na mifugo wakati wa kiangazi. Aidha wazee wa jamii ya maasai walishiriki utabiri wa kitamaduni huku wataalamu wakitoa utabiri rasmi za kisayansi za hali ya anga.