Wakulima na wafugaji wahamasishwa kuhusu haki za punda

  • | Citizen TV
    456 views

    Wanaibiwa, wanadhulumiwa na hata kuchinjwa kwa minajili ya nyama na ngozi yao. Nazungumzia punda ambaye haki zake Mara nyingi husahaulika. Kulingana na sensa ya humu nchini, takriban punda milioni moja pekee ndio waliosalia. Huku sherehe za kuadhimisha siku maalum iliyotengwa kuwakumbusha Wakulima na wafugaji kuhusu haki za punda na jinsi ya kumtunza ili awafae zikifanyika hii leo kote nchini. Kaunti ya Homabay ni mojawapo ya kaunti zilizo na idadi kubwa ya punda nchini kando na kaunti za Kitui na Turkana.