Wakulima wa miwa walalamika Busia

  • | Citizen TV
    392 views

    Wakulima wa miwa kutoka kaunti ya Busia sasa wanaitaka serikali kusitisha mpango wa kufunga viwanda saba vya sukari kwa madai ya ukosefu wa miwa, wakisema kuwa wana miwa ya kutosha . Wakulima hao, wanasema kuwa mpango huo utawaacha njia panda kwa miezi mitatu haswa wakati huu ambapo gharama ya maisha imepanda maradufu huku wakihofia kuwa mazao yao yataharibikia shambani. Hata hivyo, bodi ya sukari nchini imesema kuwa kampuni hizo hazitasaga sukari kwa miezi mitatu wakiwataka wakulima kuwa na subira.