WAKULIMA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA KILIMO CHA SOYA KUKABILI UHABA MKUBWA NCHINI

  • | KNA Video
    8 views
    Wakulima kote nchini wamehimizwa kuchangamkia kilimo cha soya ili kukabili uhaba mkubwa wa zao hilo, ambao kwa sasa unasababisha Kenya kutegemea uagizaji kutoka mataifa jirani kama Uganda na Zambia. Licha ya nchi kuhitaji zaidi ya tani 200,000 za soya kila mwaka, inazalisha takribani tani 2,000 pekee hii ikiwa ni upungufu wa zaidi ya asilimia 90