- 319 viewsDuration: 1:46Wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma wamesisitiza kuwa hawatasitisha mgomo wao hadi pale serikali itakubali kuwalipa pesa zao kulingana na mkataba wa mwaka wa 2001 hadi 2025. Wahadhiri hao wamesema watahakikisha masomo yamesitishwa katika vyuo vikuu vyote vya umma ili kushinikiza serikali na hasa wizara ya elimu kushughulikia matakwa yao. Huku mgomo huo ukiingia mwezi wa pili wiki hii, wanafunzi wameendelea kutaabika katika vyuo vikuu vya umma kwa kukosa masomo muhimu. Wizara ya elimu kufikia sasa haijaonyesha dalili zozote za kutaka kufanya mazungumzo na wakuu wa vyama vya wahadhiri wa vyuo vikuu jambo ambalo linatilia shaka iwapo kutakuwa na maafikiano hivi karibuni.