Walimu wakuu wa shule za upili za umma kuhojiwa na bunge

  • | KBC Video
    7 views

    Walimu wakuu wa shule za upili za umma wanatarajiwa kufika mbele ya kamati ya bunge ya elimu na utawala ili kujibu maswali yaliyoibuliwa na ukaguzi wa matumizi ya fedha katika shule hizo. Hii ni baada ya mhasibu mkuu wa serikali kuahidi kuwasilisha bungeni ripoti za ukaguzi wa matumizi ya fedha katika shule 450 za upili za umma katika muda wa wiki mbili zijazo kwa uchunguzi zaidi. Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya uwekezaji wa umma kuhusu elimu na utawala Wanami Wamboka amesema kamati hiyo itaanza kwa kuzingatia ripoti za ukaguzi wa shule za upili za kitaifa. Mhasibu mkuu wa serikali Nancy Gathungu alikutana na kamati leo ambapo alisema shule zote 9,000 za sekondari za umma zitakaguliwa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive