- 488 viewsDuration: 3:00Muungano wa walimu wa shule za upili nchini kuppet, umetoa ilani ya siku saba ya mgomo wakilalamikia mpango wa bima ya afya ya sha. Walimu hawa wanasema kuwa wamehangaika tangu walipohamishwa kwenye bima hii ya serikali. Wanalalamikia miongoni mwa matatizo mengine gharama ya chini ya matibabu, hitilafu za mara kwa mara na hospitali chache zinazotoa huduma kwao.