Walimu wamuonya Rais Ruto dhidi ya kukaidi maagizo yaliyotolewa na mahakama

  • | K24 Video
    119 views

    Mgogoro kati ya walimu wa tarajali wa shule za daraja la chini za sekondari na tume ya kuwaajiri walimu TSC huenda ukatatiza shughuli za mazomo kote nchini iwapo walimu hao wataendelea na mpango wa kugoma wiki ijayo. Walimu hao wamemuonya rais William Ruto dhidi ya kukaidi maagizo yaliyotolewa na mahakama katika kesi ya kupinga kuendelezwa kwa kandarasi zao za mafunzo kazini. Walimu hao wameishutumu serikali kwa kile wanachokitaja kama ubaguzi, wakiapa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya afisa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia.