Walimu wengi nchini wanakabiliwa na hali ngumu ya kifedha na kuishi kwa madeni, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na chama cha walimu wa shule za msingi KNUT. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa asilimia 97 ya walimu wa shule za msingi wanashindwa kuweka akiba kutokana na gharama kubwa za maisha na mishahara isiyotosha.
Aidha, imeripotiwa kuwa baadhi ya walimu wanapitia msongo wa mawazo unaotokana na changamoto hizo za kifedha, hali inayowafanya wengine kuwa katika hatari ya kufikia mawazo ya kujidhuru. Walimu wanasema kuwa licha ya hali hiyo, wengi wanaendelea kujikaza na kuishi kwa mikopo ili kuhimili maisha ya kila siku.mii.