Skip to main content
Skip to main content

‘Walinipiga risasi na kunitelekeza wakidhani nimekufa’

  • | BBC Swahili
    16,340 views
    Duration: 2:03
    Edgar Mwakabela maarufu Sativa anadai kutekwa Juni 2024 nchini Tanzania, baada ya kile alichodai kuwa kuikosoa serikali kuhusu masuala ya kikodi na kuunga mkono mgomo wa wafanyabiashara uliolenga kudai haki. Sativa anadai kuwa aliteswa kisha kutelekezwa kwenye msitu baada ya kupigwa risasi. Watetezi wa haki wameeleza kuwa wanaharakati na wanasiasa wa upinzani wanapotea, wengi wao hawarudi tena na iwapo watapatikana watakuwa na simulizi za kutisha. Serikali ya Tanzania imekanusha kuhusika na matukio ya watu kupotea. BBC ilituma maombi ya mahojiano na polisi lakini haikujibiwa. Taarifa imeandaliwa na Alfred Lasteck. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw