Walioathirika na Bajeti I Wapenzi wa kamari na vileo wakikaza kamba kiunoni

  • | KBC Video
    26 views

    Wananchi ni miongoni mwa washinde katika mapendekezo ya bajeti ya mwaka huu kufuatia nyongeza ya ushuru wa thamani kwa bidhaa za mafuta kutoka asilimia 8 hadi asilimia 16, inayotarajiwa kuathiri bei za bidhaa na utoaji huduma. Waziri wa fedha Profesa Njuguna Ndung’u ameongeza mifumo mitatu ya ushuru kwa wale wanaopokea mshahara wa kati ya shilingi elfu 18 na elfu 24 ambao hawakuwa wakitozwa ushuru huo lakini sasa watatozwa ushuru. Wanaopokea mshahara wa zaidi ya nusu milioni ambao walikuwa wakilipa asilimia 30 ya ushuru wa mshahara, sasa watalipa asilimia 32 ilhali wanaopokea zaidi ya shilingi laki 8 watatozwa ushuru wa asilimia 35.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channell: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #budget2023 #darubini