Wanabodaboda wawalipia karo wasichana Homa Bay

  • | Citizen TV
    773 views

    Kikundi cha waendeshaji bodaboda katika eneo bunge la Rangwe kaunti ya Homabay kimejitokeza kufadhili masomo ya zaidi ya wanafunzi 100 wasichana katika shule mbalimbali za eneobunge hilo. Aidha wamechukuwa jukumu la kuwapeleka na kuwarudisha wasichana wanaotoka mbali kuenda shuleni bila malipo kama njia moja ya kuwapa motisha kwenye masomo. James latano anatuarifu zaidi kutoka Homa-Bay.