Wanachama wa Ford-Kenya wapinga kuvunja chama wala kujiunga na chama cha UDA

  • | Citizen TV
    409 views

    Wanachama wa FORD-Kenya Tawi la Garissa wamepinga vikali pendekezo la kutaka vyama vyote chini ya muungano wa Kenya Kwanza kuvunjwa na kujiunga na chama cha UDA. Wanachama hao wanasema maoni hayo yanayopigiwa debe na katibu mkuu wa UDA Cleophas Malala yatahujumu demokrasia ya vyama vingi nchini. Wakiongozwa na mwenyekiti wao Mohamed Timaged, wanasiasa hao wanasema uhuru wa vyama utaathirika na kukosa kunawiri iwapo pendekezo hilo litapitishwa