- 367 viewsDuration: 3:06Takriban wanafunzi 57,000 wamekosa nafasi katika vyuo vikuu nchini, kulingana na Taasisi ya Uteuzi wa Wanafunzi kwa Elimu ya Juu (KUCCPS). Taasisi hiyo imesema kuwa karibu wanafunzi 6,500 waliomba kozi za udaktari ilhali nafasi zilizokuwepo zilikuwa 702 pekee. Aidha, idadi kubwa ya waombaji ilichagua kozi za ualimu. Na kama anavyoarifu Brenda Wanga, Wizara ya Elimu imesema itafungua dirisha jingine la kutuma maombi kwa wanafunzi ambao hawakufanikiwa kutuma maombi katika awamu ya kwanza.