Wanafunzi wa kike huko Siaya watatizika na ukosefu wa sodo

  • | Citizen TV
    56 views

    Ukosefu wa sodo ni mojawapo ya vikwazo vinavyoathiri pakubwa wasichana wanaoishi katika umasikini katika kaunti ya Siaya, idadi yao kubwa ikilazimika kusalia nyumbani punde wanapoanza kupata hedhi. Hata hivyo zaidi ya wanafunzi 1500 kutoka shule mbalimbali za wasichana na za kutwa katika kaunti hiyo wanasababu ya kutabasamu baada ya baadhi ya mashirika ya kijamii kushirikiana kuzindua mpango wa kuwapa sodo wasichana wanaotoka familia zisizojiweza. Akizungumza katika shule ya wasichana ya Sinaga, mkurugenzi mkuu wa Together for Better Foundation, Aruna Varsani, ameeleza kuwa tayari zaidi ya wasichana elfu thelathini kaunti nyingine 24 wamenufaika na mpango huo uliaonzishwa mwaka wa 2020. Shughuli hiyo inayotarajiwa kufanyika kwa wiki moja inalenga kuwapa mafunzo wanafunzi hao kuhusu usafi wa hedhi.