Wanafunzi wa kike waraiwa kukumbatia masomo ya sayansi

  • | Citizen TV
    243 views

    Licha ya uhaba wa wanafunzi wa kike wanaosoma masomo ya sayansi nchini, wanafunzi wamehimizwa kukumbatia masomo hayo katika kaunti za kirinyaga na kakamega. Mkurugenzi mkuu wa vyuo vikuu humu nchini Dkt. Mercy Wahome ambaye ameelezea kuwa asilimia sita tu ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kcse mwaka jana ndio waliohitimu kundelea na na masomo ya sayansi. Inaarifiwa kuwa kinachosababisha kuwepo kwa uhaba wa wanafunzi wa kike wanaofanya masomo ya sayansi ni dhana potovu. Rai hizo pia zimetolewa kwa wanafunzi katika kaunti ya Kakamega.