Wanafunzi wa vyuo vikuu wataja sintofahamu kuhusu mwongozo mpya wa karo

  • | Citizen TV
    220 views

    Wasiwasi imegubika maelfu ya wanafunzi wa vyuo vikuu na wazazi wao majuma kadhaa baada ya wizara ya elimu kutangaza kupunguza karo kwa kati ya asilimia 15 na 40. Hata hivyo wengi wanasema bado hawajapata muongozo wa karo kutoka kwa serikali ili kujipanga mapema. Hata hivyo, waziri wa elimu Migos Ogamba ameondolea mbali wasiwasi akisema barua za karo mpya zitawafikia wanafunzi juma hili