- 816 viewsDuration: 3:32Saa chache baada ya wizara ya elimu kutangaza kuongezwa kwa muda wa kusajili wanafunzi wa Gredi ya 10 katika shule mbalimbali nchini, wazazi wengi wanasema tatizo kubwa si muda ila ukosefu wa pesa ndio unawasababisha kusalia na wana wao nyumbani. Runinga ya Citizen imepiga darubini maeneo mbalimbali na kuzungumza na wazazi kuhusu uhalisia wa mambo vijijini. Chrispine Otieno alitangamana na baadhi ya wazazi na watoto waliosalia nyumbani na hii hapa taarifa yake.