- 1,808 viewsDuration: 2:51Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetang'ula, anaendelea kujipata mashakani kisheria baada ya wanaharakati kurejea mahakamani wakitaka akamatwe kwa madai ya kukaidi amri ya mahakama. Shirika la kutetea haki za binadamu, Vocal Africa, linasema licha ya uamuzi wa Mahakama Kuu uliowataka Wetang'ula na mwenzake wa Seneti, Amason Kingi, kujiepusha na shughuli za kisiasa, spika huyo ameendelea kushiriki kampeni na mikutano ya kisiasa. Wanaharakati hao wanadai hatua hizo zinakiuka amri ya mahakama na wanataka sheria ichukue mkondo wake.