Wanakriminolojia warai ushirikiano wa taasisi za haki

  • | Citizen TV
    215 views

    Muungano wa wanakriminolojia Nchini (PCAK) umeomba ushirikiano kati ya taasisi zinazojihusisha na masuala ya haki kwenye vita dhidi ya uhalifu. Wakizungumza Meru kwenye hafla ya kuzindua Muungano huo ukanda ya Mlima Kenya Mashariki, wamezitaka asasi kama vile IPOA, DCI na idara ya Mahakama kuhakikisha wahalifu wanapokamatwa, kesi hizo zinafuatiliwa hadi tamati na haki inatendeka. Muungano huu unahusisha wafanyikazi wa serikali na sekta za kibinafsi zinazopambana na uhalifu Nchini.