Wanaoishi kwenye ardhi Kirima huko Njiru wapata afueni ya muda

  • | Citizen TV
    2,595 views

    Ni afueni kwa mamia ya wakaazi wanaoishi katika ardhi inayomilikiwa na familia ya aliyekuwa mbunge wa Starehe Gerishon Kirima baada ya mahakama kuu kutoa agizo kusitisha kufurushwa kwao. Mahakama kuu sasa ikitarajiwa kutoa uamuzi wake tarehe 29 mwezi Januari. Na kama Ben Kirui anavyoarifu, agizo hili linajiri siku moja tu baada ya wizara ya ardhi kusema kuwa wanaoishi hapo watalazimika kujipanga.