- 1,085 viewsDuration: 2:48Wanariadha walioshiriki kwenye mashindano ya dunia mjini Tokyo Japan walikaribishwa kwa mbwembwe nchini baada ya kuiweka Kenya kwenye nafasi ya pili katika mashindano hayo. Mashujaa hao wa taifa wanarejea nchini na jumla ya medali 11, saba zikiwa za dhahabu. Haya ni huku wabunge wakiwamiminia sifa kedekede wanariadha hao huku wakiibua maswali kuhusu matokeo duni ya wanaume kwenye mbio hizo.